Nenda kwa yaliyomo

Bustani ya Menara

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Bustani ya Menara ni bustani ya umma ya kihistoria ndani ya mji wa Marrakesh nchini Moroko. Ilianzishwa kwenye karne ya 12 mnamo mwaka 1157 wakati wa ukhalifa wa Wamuwahidun(Almohadi) chini ya mtawala Abd al-Mu'min. Pamoja na bustani ya Agdal na mji wa kihistoria wa Marakesh, bustani zimeorodheshwa na UNESCO kama Urithi wa Dunia tangu mwaka 1985.[1]

Bustani ilipangwa ikizunguka beseni kubwa ya maji na kando yake kipo kibanda cha starehe. Bustani yote pamoja na kibanda cha starehe kilichopo mbele ya mandhari na nyuma ya milima ya Atlas na hivyo kuzingatiwa mojawapo ya ishara za Marrakesh.[2]: 282 

  1. Centre, UNESCO World Heritage. "Medina of Marrakesh". UNESCO World Heritage Centre (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-01-27.
  2. Wilbaux, Quentin (2001). La médina de Marrakech: Formation des espaces urbains d'une ancienne capitale du Maroc. Paris: L'Harmattan. ISBN 2747523888.
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Bustani ya Menara kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  翻译: