Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kiukraini
Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kiukraini ilikuwa kati ya jamhuri wanachama 15 za Umoja wa Kisovyeti hadi mwaka 1991.
Jina lake liliandikwa kwa alfabeti ya Kisirili katika lugha ya Kiukraini: "Українська Радянська Соціалістична Республіка, УРСР" (Ukrainska Radyanska Sotsialistichna Respublika, URSR) na pia kwa Kirusi "Украинская Советская Социалистическая Республика" (Ukrainskaya Sovyetskaya Sotsialisticheskaya Riespublika, USSR).
Mji mkuu wa kwanza ulikuwa Kharkiv lakini serikali ilihamia Kiev mwaka 1934.
Jamhuri hii ilikuwa moja ya nchi wanachama walioanzisha Umoja wa Mataifa.[1] Hali halisi haikuwa na madaraka ya pekee kwa sababu ilikuwa chini ya usimamizi wa serikali kuu ya Moscow.
Baada ya kuporomoka kwa Umoja wa Kisovyeti nchi ilipata uhuru wake na kuwa nchi Jamhuri ya Ukraini.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Activities of the Member States - Ukraine". United Nations. Iliwekwa mnamo 2011-01-17.