Nenda kwa yaliyomo

Mnyama

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wanyama
Wanyama mbalimbali; kutoka juu-kushoto mpaka chini-kulia: kiti cha pweza, sifongo-bahari, ngisi kibete, konyeza, nondo-chui, mwata, kombe-taa, chui milia, mfoko-bahari, kidudu-dubu, mnyama-kigoga, mkunga-chui, kaa, daa kichwa-miiba, kunguru buluu, buibui mrukaji, mnyoo-bapa bahari, daa-upepeo.
Uainishaji wa kisayansi
Domeni: Eukaryota
Himaya: Animalia
Linnaeus, 1758
Ngazi za chini

Faila:

Wanyama (jina la kisayansi ni animalia na hutoka katika Kilatini) ni viumbehai wasio mmea, kuvu, bakteria, protista au arkea. Vile vile tunaweza kusema wanyama ni viumbehai wanaotegemea chakula kutoka sehemu nyingine: wao hawana uwezo wa kujitengenezea chakula chao wenyewe kupitia usanisinuru (nishati ya jua) lakini kutoka kwa viumbehai vingine ama wanyama wengine au mimea.

Kufuatana na aina ya chakula tunatofautisha hasa wanaokula mimea wanaoitwa walamani au walamea (kwa Kiingereza: herbivorous) na wanaokula nyama wanaoitwa walanyama au wagwizi (ing. carnivorous). Kuna pia walavyote (ing. omnivorous) wanaoweza kula kila kitu, ama mimea ama wanyama wengine (ing. omnivorous).

Wanyama wanahitaji oksijeni kwa kupumua.

Wanyama walio wengi hutembea yaani hubadilisha mahali wanapokaa, kwa hiyo wanahitaji milango ya maarifa.

Sayansi inayochunguza wanyama huitwa zoolojia, ambayo ni tawi la biolojia.

Aina za wanyama ni nyingi sana. Mara nyingi aina zao zinatofautishwa kama ni wanyama wenye seli nyingi (metazoa) au seli moja (protozoa) tu.

Kuna wanyama wanaoishi peke yao, katika vikundi na jamii. Mfano wa wanyama wanaoishi peke yao ni kifaru au nyoka. Wanajumuika kwa tendo la kuzaa pekee. Mfano wa wanyama wa jumuiya ni simba wanaokaa na kuwinda pamoja. Ushirikiano unasaidia kupata chakula bora. Mfano wa wanyama katika jamii ni nyuki na wadudu wengine.

Upande wa mwili hata binadamu ni mnyama na kimaumbile anahesabiwa kati ya mamalia.

Binadamu hutofautisha mara nyingi wanyama wakubwa zaidi, kwa kawaida wenye uti wa mgongo (kwa Kilatini: Chordata), kati ya:

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mnyama kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  1. https://www.mwananchi.co.tz/mw/habari/kitaifa/usasa-unavyowahatarisha-watu-kuambukizwa-3572078
  翻译: