Nenda kwa yaliyomo

Namibia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Republic of Namibia
Jamhuri ya Namibia
Bendera ya Namibia Nembo ya Namibia
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Unity, Liberty, Justice
Wimbo wa taifa: Namibia, Land of the Brave (Namibia, nchi ya mashujaa)
Lokeshen ya Namibia
Mji mkuu Windhoek
22°33′ S 17°15′ E
Mji mkubwa nchini Windhoek
Lugha rasmi Kiingereza1
Serikali Jamhuri
Nangolo Mbumba
Saara Kuugongelwa
Uhuru
Kutoka Afrika Kusini
21 Machi 1991
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
825,615 km² (ya 34)
kidogo sana
Idadi ya watu
 - Julai 2023 kadirio
 - 2011 sensa
 - Msongamano wa watu
 
2,777,2322 (ya 141)
2,113,077
3.2/km² (ya 235)
Fedha Namibia dollar (NAD)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC+1)
(UTC)
Intaneti TLD .na
Kodi ya simu +264

-


Namibia ni nchi ya Afrika ya Kusini kwenye pwani ya Atlantiki.

Imepakana na Angola, Zambia, Zimbabwe Botswana na Afrika Kusini.

Imepata uhuru wake kutoka Afrika Kusini mwaka 1990 baada ya vita vya ukombozi.

Mji mkuu ni Windhoek (wakazi 431,000 hivi mwaka 2020).

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]

Sehemu kubwa ya nchi ni kavu sana na jangwa za Namib na Kalahari zinafunika asilimia kubwa ya uso wa nchi.

Jangwa la Namib liko upande wa magharibi likifuata pwani ya Atlantiki kuanzia Afrika Kusini hadi Angola. Upande wa mashariki kuna jangwa la Kalahari linalovuka mpaka wa Botswana.

Katikati ya majangwa hayo kuna nyanda za juu zinazofikia kimo cha mita 1700 kwa wastani.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Historia ya kale

[hariri | hariri chanzo]

Wakazi wa kwanza huaminiwa kuwa wawindaji-wakusanyaji wa jamii ya Wasani.

Katika karne ya 14 hivi BK walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi walioshika utawala na hatimaye kuwa wengi kuliko wenyeji.

Chini ya ukoloni

[hariri | hariri chanzo]

Namibia katika mipaka ya sasa ilianzishwa katika karne ya 19 kama koloni la Ujerumani kwa jina la Afrika ya Kusini-Magharibi ya Kijerumani. Maeneo yake yaliunganishwa mara ya kwanza kwenye mwaka 1884.

Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia ilivamiwa na Uingereza na Afrika Kusini. Pamoja na makoloni mengine ya Ujerumani iliwekwa chini ya mamlaka ya Shirikisho la Mataifa. Tangu mwaka 1919 ilikuwa eneo la kudhaminiwa kwa niaba ya Shirikisho la Mataifa chini ya serikali ya Afrika Kusini.

Afrika ya Kusini-Magharibi (kwa Kiingereza South-West Africa) ilikuwa jina la eneo hilo kuanzia mwaka 1922 hadi uhuru wa nchi ya Namibia mwaka 1990.

Baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, wakati wa kuvunjwa kwa Shirikisho la Mataifa mwaka 1946, Umoja wa Mataifa ulichukua jukumu la kuratibu maeneo ya kudhaminiwa.

Afrika Kusini haikutambua badiliko hilo ikitangaza ya kwamba hali ya udhamini ilikuwa ya Afrika ya Kusini-Magharibi tangu kuvunjwa kwa Shirikisho la Mataifa.

Mwaka 1949 bunge la Afrika Kusini lilitangaza sheria ya kufanya eneo kuwa jimbo la tano la Afrika Kusini na kueneza siasa ya apartheid (ubaguzi wa rangi) hadi hukoikijaribu kulitendea eneo hilo kama sehemu kamili ya Afrika Kusini. Hii haikukubaliwa na Umoja wa Mataifa na nchi nyingi za dunia.

Baadaye mfumo wa bantustans sawa na Afrika Kusini ulianzishwa pia huko ambako maeneo makubwa yenye rutuba yalitengwa kwa ajili ya Wazungu ilhali Waafrika walitakiwa kuwa na maeneo kadhaa tu kama "homeland" walipokuwa na haki ya kukaa, lakini katika maeneo mengine waliruhusiwa kukaa kama wafanyakazi kwa muda tu. Mfumo huo haukutekelezwa kwa ukali, tofauti na Afrika Kusini yenyewe.

Hii haikukubaliwa na Umoja wa Mataifa ulioendelea kudai ya kwamba Afrika Kusini ilipaswa kuandaa eneo kwa uhuru.

Mwaka 1966 Mkutano Mkuu wa UM uliamua kuondoa mamlaka ya Afrika Kusini na kuweka eneo moja kwa moja chini ya Umoja wa Mataifa. Azimio hilO halikuweza kutekelezwa kwa sababu Afrika Kusini ilikataa.

Hapo wanamgambo wa chama cha SWAPO walichukua silaha wakajaribu kupigania uhuru.

Azimio la Mkutano Mkuu wa UM la mwaka 1968 lilibadilisha jina la eneo kuwa Namibia.

Mwaka 1971 Mahakama ya Kimataifa ya Haki ikaamua ya kwamba utawala wa Afrika Kusini si wa haki. Mwaka 1978 Umoja wa Mataifa uliamua ya kwamba Afrika ya Kusini-Magharibi unapaswa kupewa uhuru. Hapo serikali ya Afrika Kusini ikaanza kuchukua hatua za kuandaa uhuru wa eneo hili, lakini vita kati ya jeshi lake, SWAPO na wanajeshi wa Angola na Kuba iliendelea.

Baada ya miaka ya vita vya kupigania uhuru, mchakato wa kimataifa wa kuelekea uhuru ulianza na kufikia mapatano ya kumpumzisha silaha mwaka 1988. Hatimaye mwaka 1990 nchi ilipata uhuru wake kwa jina la Namibia.

Wakazi wengi ni wa makabila ya Wabantu, hasa Waovambo (49.5%). Pia wako wengi wa jamii ya Wakhoisan, ambao wametokana na wenyeji wa nchi. Asilimia 4 - 7 wana asili ya Ulaya, hasa Makaburu na Wajerumani, na asilimia 8 ni machotara.

Upande wa lugha, Oshiwambo ni lugha ya kwanza ya karibu nusu ya wakazi, lakini Kiingereza ndicho lugha rasmi ingawa ni lugha ya kwanza ya 3% pekee za wakazi. (Angalia Orodha ya lugha za Namibia.)

11.3% za wakazi wanatumia lugha za Kikhoisan.

Kijerumani na Kiafrikaans zilikuwa lugha rasmi pamoja na Kiingereza hadi uhuru. Wakazi wengi hutumia Kiafrikaans kama lugha ya pili, na 10.4% kama lugha ya kwanza.

Wakazi wenye asili ya Ulaya huongea kama lugha ya kwanza Kiafrikaans (60%), lakini pia Kijerumani (32%) na Kireno (4-5%), hasa wenye asili ya Angola.

Upande wa dini, 87.9% za wakazi ni Wakristo (hasa Walutheri ambao ni 43.7%; Wakatoliki ni 22.8%, Waanglikana ni 17%). Waliobaki kwa kawaida wanafuata dini asilia za Kiafrika (10.2%).

Picha za Namibia

[hariri | hariri chanzo]

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Serikali
Elimu
Rushwa
Utalii
Kulinda amani


Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Namibia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  翻译: