Nenda kwa yaliyomo

Uwanja wa Ndege wa Wilson (Kenya)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kigezo:Infobox airport

Fokker 50.

Uwanja wa Ndege wa Wilson uko kilomita tano kusini mwa jiji la Nairobi, Kenya, karibu na vitongoji vya Langata, South C na Kibera.

Uwanja huo wa ndege umekuwa ukitumika tangu 1933. Ulikuwa uwanja mkuu wa ndege hadi kufunguliwa kwa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta. Uwanja huo wa ndege unatumika kwa safari za kimataifa pamoja na za ndani ya nchi. Inatumika zaidi na ndege ndogo. Sekta zinazotumia huduma zake sana ni za utalii, huduma za afya na kilimo. Uwanja huo wa ndege una wastani ya 120,000 ya ndege zinazoshuka na kupaa kwa mwaka. Airkenya na kampuni nyingine ndogo za ndege zinatumia uwanja wa Wilson kwa huduma za abiria za ndani ya nchi, badala ya Uwanja wa Jomo Kenyatta ambao ni uwanja mkuu wa ndege jijini Nairobi. Wamisionari wanaohudumu ndege kama AMREF, MAF na AIM AIR hutumia uwanja wa Wilson kama wigo wao wa Afrika. Uwanja huo wa ndege hutumiwa pia kwa mafunzo ya urubani. "Kenya Airports Authority" (KAA) viwanja vya Ndege ya Kenya ndio imedhibitiwa na mamlaka ya kuendesha uwanja huu wa ndege.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Uwanja huu wa ndege awali ulianzishwa mnamo mwaka wa 1933 kama Nairobi Aerodrome, na ulikuwa ukitumika kwa usafirishaji wa angani wa barua na shirika la ndege la Imperial. Uwanja huo mara ukabadilishwa jina kuwa uwanja wa ndege wa Wilson mwaka wa 1962. Uwanja huo umechukua jina la Bibi Florence Kerr Wilson, mmoja wa waanzilishi wa usafiri wa angani nchini Kenya.

Kampuni za Ndege na Sehemu za Usafiri

[hariri | hariri chanzo]
Shirika la Sehemu ya Usafiri Destination
Aero Kenya Eldoret
Airkenya Express Amboseli, Kilimanjaro, Lamu, Lewa Downs, Malindi, Masai Mara, Meru, Mombasa, Nanyuki, Samburu
ALS - Aircraft Leasing Services Loki, Rumbek, Juba
Blue Bird Aviation (Kenya)
Delta Connection (Kenya) Juba, Yei, Rumbek
Safarilink Aviation Safarilink Aviation

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
  翻译: