Tanzania Agricultural Development Bank’s Post

Kama msemo wa Kiswahili usemavyo, Samaki mkunje angali mbichi hivyo ndivyo TADB kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha wanavyofanya kwa kutoa elimu ya fedha kwa wanafunzi wanaohudhuria kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayoendelea mkoani Mbeya, Viwanja vya Ruanda Nzovwe. Wanafunzi hao wamejifunza mambo mbalimbali ikiwemo umuhimu wa kutumia huduma rasmi za fedha, matumizi sahihi ya fedha, umuhimu wa kuweka akiba na namna ya kujitengenezea bajeti. Pamoja na hayo walipata kuifahamu Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) namna inavyofanyakazi katika kuchagiza mageuzi ya kilimo nchini kutoka kilimo cha kujikimu kwenda kilimo cha kibiashara. #TADB #KilimoKinaBenkika #WikiyaHudumazaFedha2024 #Mbeya

  • No alternative text description for this image
  • No alternative text description for this image
  • No alternative text description for this image
  • No alternative text description for this image
  • No alternative text description for this image
    +4

To view or add a comment, sign in

Explore topics