Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe, Bi. Happiness Seneda aialika TADB mkoani Songwe kujionea fursa za kilimo na kujadili namna bora ya kufikisha mikopo ya kilimo kwa wananchi alipotembelea banda la Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayofanyika katika Viwanja vya Ruanda-Nzovwe, Jijini Mbeya. Katika banda la TADB Bi. Happiness Seneda, alipata maelezo kuhusu Huduma za TADB, Mfuko wa Dhamana wa Wakulima Wadogo - SCGS na namna unanavyofanyakazi kwa kushirikiana na mabenki ya kibiashara na taasisi za kifedha katika kuchagiza mageuzi ya kilimo nchini kutoka kilimo cha kujikimu kwenda kilimo cha kibiashara. #TADB #KilimoKinaBenkika #WikiyaHudumazaFedha2024 #Mbeya
-
-
-
-
-
+2