Watu wanataka kuwa sehemu ya kile ambacho kila mtu anakifanya.

Watu wanataka kuwa sehemu ya kile ambacho kila mtu anakifanya.

Umeshawahi kujiuliza kwa nini unajikuta unanunua kitu tu sababu watu wengine walifanya hivyo?

Au unajikuta unakula kwenye mgahawa ambao watu wengii wanauzungumzia na wanaenda huko, hata kama hujui chakula chao kikoje?

Kuna psychology nzito hapo, na wala siyo bahati mbaya.

Sasa, unawezaje kuvuta wateja wako kwenye biashara yako hadi wafikirie wanahitaji kitu hata kama walikuwa hawajakitaka dakika kumi zilizopita?

Ngoja nikupe siri...

➡️ Uthibitisho wa jamii (Social Proof )⬅️

Ndio, usitishwe na jina hilo – Social Proof ni silaha ya siri inayokusaidia kufanya watu waseme, “Nataka hicho kama alicho chukua yule!”


Kwenye kitabu chake maarufu, "Influence: The Psychology of Persuasion, Robert Cialdini" anaelezea jinsi biashara zinavyoweza kushawishi watu kutumia athari hii ya kisaikolojia.

Wasanii wa Bongo Flava kwenye Boomplay

Ukiangalia Boomplay utaona pamejaa "Most Played" na "Top Trending" kila kona. Sio lazima ufikirie mara mbili kabla ya ku-play wimbo mpya wa Diamond Platnumz – kama kila mtu anaskiliza, lazima na wewe usikilize! Hii inaitwa FOMO (Fear Of Missing Out) ,watu wanaogopa kupitwa na wakati hivyo hupendelea vile vitu ambavyo watu wengi huvifuatilia na Boomplay wanatumia vyema.


Jinsi Biashara za Kibongo Zinavyotumia Social Proof Kushinda Wateja:

Biko Jackpot | Kila Mtu Anafaidi, Na Wewe Je?

Tuseme ukweli, Biko inakufanya uhisi utafaidi jackpot kwa sababu unaona watu wameshika zile cheki kubwa za ushindi. Ni mbinu ya kawaida lakini inafanya kazi.


Chukua hii!

Onyesha kwamba kila mtu anatumia bidhaa yako, Unaweza kupost screenshots za malipo halisi kutoka kwa wateja wako waliolipa. Ukifanya hivi, kila mtu ataona kwamba kuna watu wengi wanapata bidhaa yako.

Mfano: Post picha/videos kuonyesha wateja wengi wanakuja au wananunua kutoka kwako. Kama umepost bidhaa, waonyeshe kama mzigo umenunuliwa wote, post ushahidi, post screenshot za ushuhuda kukoka kwa wateja wako, waonyeshe watu kua " Kila mtu anatumia bidhaa hii, bado wewe tu"

Watu wanaona na wanapata hiyo hamu ya kununua pia. Ni kama vile wanashawishika kwamba, "Kama kila mtu anapata, mimi pia lazima nipate."

Thanks for reading! Subscribe for free to receive new posts and support my work.        

To view or add a comment, sign in

Explore topics